Kichwa
cha uvumbuzi: Procuc System
Jina la mvumbuzi: Marco Shigele
MAELEZO
YANAYOHUSU UVUMBUZI
Utangulizi
Mfumo
wa Procuc ni mfumo mpya kabisa utakaokuwa msaada mkubwa sana
katika biashara za ndani na nje. Mfumo huu utashawishi watu wengi sana kujiunga
ili kuweza kushiriki kikamilifu katika shughuli za uzalishaji.Wafanyabiashara
wengi wataweza kupata fedha kwa ajili ya kukuza mitaji bila kukopa fedha kutoka
taasisi yoyote ya fedha.Kwa hiyo watu watapata fursa ya kupata fedha kwa ajili
ya kukuza mitaji yao bila dhamana ya kitu kisichohamishika.Mfumo wa Procuc ni
tofauti kabisa na Upatu, kwa kuwa mfumo unamfanya mtu aweze kushiriki katika
shughuli za uzalishaji badala ya kuchangiana pesa ambayo haitumiki moja kwa
moja kwenye mzunguko wa kibiashara.Mfumo unalenga hasa kuwasaidia
wafanyabiashara ambao hawana uwezo wa kukopa benki au taasisi yoyote ya fedha
kwa kigezo cha dhamana ya kitu kisichohamishika. Pia mfumo huu unafaa hata kwa
wafanyabiashara wenye uwezo wa kukopa benki au taasisi yoyote ya fedha.Vilevile,
hata watu ambao si wafanyabiashara wataweza kupata mitaji kwa ajili ya kufanya
biashara au kutekeleza malengo waliojiwekea kupitia mfumo huu.Mfumo wa Procuc
unaweza kuwa hatua stahiki ya kuchukua kwa lengo la kupunguza umaskini kwa
kuongeza uzalishaji,kuboresha huduma na kukuza ajira. Ikumbukwe kuwa mfumo huu
hautaathiri kabisa shughuli za kibenki, badala yake utaiongezea benki wateja
wenye sifa za kukopa kulingana na masharti ya kibenki na pia mfumo utaongeza
uwezo na kasi ya kukuza uchumi wa Nchi.
Malengo
ya mfumo wa Procuc
Mfumo wa Procuc una
malengo yafuatayo:
·
Kuongeza mtaji kwa biashara ambayo mtaji
wake haukidhi haja ya wateja bila kukopa benki kwa kigezo cha dhamana ya kitu
kisichohamishika.
·
Kuwawezesha watu wenye mtaji mdogo kuwa
na uwezo wa kufanya biashara.
·
Kuwawezesha wafanyakazi ambao hawana
muda wa kufanya biashara kwa sababu ya kubanwa na shughuli za kiofisi kuongeza
kipato chao huku wakiendelea kufanya kazi.
·
Kuwanasua watu kutoka katika matumizi
mabaya ya fedha.
·
Kuwashawishi watu wengi kushiriki katika
shughuli za uzalishaji.
Matazamio
ya Mfumo wa Prokak kwenye jamii
·
Mfumo unaweza kuzidisha umakini na
uwajibikaji katika biashara.
·
Mfumo wa Procuc unaweza kuwa hatua
stahiki ya kuchukua kwa lengo la kupunguza umaskini.
Dhana
inayohusu mfumo wa Procuc
Mfumo wa Procuc ni njia
inayotumika katika biashara ambayo inahusisha mwenye mali (Procuc Operator),
mwenye hela (Customer) na mteja (Client). Jina Procuc limetokana na majina
matatu yaliyotoholewa kutoka Lugha ya Kingereza ambayo ni Proprietor, Customer na Client.
Herufi tatu za mwanzo (Pro)
zinatokana na herufi tatu za mwanzo za jina Proprietor,
cu inatokana na herufi mbili za
mwanzo za jina Customer na c inatokana na herufi ya mwanzo ya jina Client.Kwa hiyo, Pro, cu and c
kwa pamoja zinaunda jina Procuc. Mwenye mali, mwenye hela na
mteja kwa pamoja wanajulikana kwa jina la wahusika wa mfumo wa Procuc. Elimu
inayohusu mfumo wa Procuc inaitwa Procuciology.
Mtu anayejifunza mambo yanayohusu Procuciology
anaitwa Procuciologist.Mwanzilishi
wa mfumo wa Procuc anaitwa Procusysiator.
Wadau
wa Mfumo wa Procuc
Kuna wadau watatu wa
mfumo wa Procuc, ambao ni:-
·
Mwenye mali
·
Mwenye hela
·
Mteja
Mwenye
mali
Katika mfumo wa Procuc,
mwenye mali ni mtu anayeendesha biashara halali.Jina biashara katika mfumo huu linajulikana kwa jina la Procuc.Kwa hiyo, mwenye mali ni mtu
ambaye anaendesha Procuc, pia ndiye mtu pekee anayetambuliwa rasmi katika
uendeshaji wa Procuc.Procuc ni biashara inayofanyika kwenye mfumo wa Procuc au
ni biashara yoyote au kitega uchumi chochote au mradi wowote ambao unaweza kuzalisha kiasi kikubwa cha faida
kutokana na mtaji uliowekezwa. Mwenye mali ni mhusika wa kwanza wa mfumo wa
Procuc.
Mwenye hela
Mwenye hela ni mtu
ambaye anaongeza hela (mtaji) kwenye mtaji wa mwenye mali ili kuweza kuendesha
Procuc. Inawezekana kabisa kwa mwenye mali kuwa na watu (wenye hela) wengi wa kumchangia mtaji.Mwenye
hela ni mhusika wa pili wa mfumo wa Procuc.
Mteja
Mteja ni mtu anayenunua
bidhaa kwenye Procuc. Wateja wamegawanyika katika sehemu kuu mbili yaani wateja
wa kwanza (umoja: mteja wa kwanza) na wateja wa pili (umoja: mteja wa
pili).Mteja wa kwanza ni yule ambaye ananunua bidhaa kutoka kwa Pocu.Pocu ni jina la pamoja
linalojumuisha , mwenye mali na mwenye hela.Kwa hiyo mtu akisema Pocu atakuwa
ametaja majina mawili kwa pamoja, yaani mwenye mali na mwenye hela. Mteja wa
kwanza kwa Pocu anaweza kuwa mwenye mali au baadaye akawa mwenye mali.Mteja wa
pili ndiye mtumiaji wa mwisho wa bidhaa. Mteja ni mhusika wa tatu wa mfumo wa
Procuc.
MWINGILIANO WA PROCUC
Mwingiliano wa Procuc
(kwa kifupi mno, imeelezwa zaidi kwenye kitabu) unaonesha jinsi mwenye mali na mwenye hela, mwenye mali
na mteja wa kwanza, mwenye mali na mteja wa pili, Pocu na mteja wa kwanza, Pocu
na mteja wa pili, mteja wa kwanza na mteja wa pili wanavyoweza kuhusiana katika
kufanya biashara. Mwingiliano wao una faida kwa kila mmoja. Kuna aina sita za
mwingiliano wa Procuc, aina hizo ni:-
·
Pocuism
·
Poconism
·
Poctism
·
Clieontism
·
Pocuclieonism
·
Pocuclientwism
Pocuism
Pocuism ni mwingiliano
kati ya mwenye mali na mwenye hela.Mwenye hela atapata fedha kutoka kwa mwenye
mali. Fedha hiyo itatokana na kiasi cha hela ambacho yeye atakuwa amechangia
kwenye Procuc. Mwenye mali atapata pesa kutokana na faida ya mtaji ambao Mwenye
hela atakuwa amechangia kwenye Procuc.
Poconism
Poconism ni mwingiliano
kati ya mwenye mali na mteja wa kwanza. Mteja wa kwanza atapata manunuzi kutoka
kwa mwenye mali.
Poctism
Poctism ni mwingiliano
kati ya mwenye mali na mteja wa pili. Mteja wa pili atapata manunuzi kutoka kwa
mwenye mali.
Clieontism
Clieontism ni mwingiliano
kati ya mteja wa kwanza na mteja wa pili. Mteja wa pili atapata manunuzi kutoka
kwa mteja wa kwanza.
Pocuclieonism
Pocuclieonism ni mwingiliano
kati ya Pocu na mteja wa kwanza. Mteja wa kwanza atapata manunuzi kutoka kwa
Pocu.
Pocuclientwism
Pocuclientwism ni mwingiliano
kati ya Pocu na mteja wa pili. Mteja wa pili atapata manunuzi kutoka kwa Pocu.
Masharti
ya kuendesha Procuc
Ikumbukwe kuwa si kila
biashara inafaa kuendeshwa kama Procuc wala si kila sehemu inafaa kwa Procuc.
Vilevile si kila mtu anafaa kuwa mwenye mali.Kwa hiyo, Procuc inategemea mwenye
mali, sehemu husika, mazingira ya kibiashara na aina ya biashara.Kwa
sasa, katika kitabu cha Procuc System, kuna masharti kumi na saba yanayohusu
uendeshaji wa Procuc.Masharti haya yana ainisha mambo manane ya msingi kama
ifuatavyo:-
·
Sifa za mtu kuwa mwenye mali.
·
Sifa za mtu kuwa mwenye hela.
·
Mazingira ya kuendeshea Procuc.
·
Sifa ya Procuc.
·
Utaratibu wa malipo.
·
Muda wa kuendesha Procuc.
·
Utaratibu wa mtu kuwa mwenye hela.
·
Ukiukwaji wa mkataba baina ya mwenye
mali na mwenye hela.
Kanuni za kihisabati
Kuna kanuni mpya za
kihisabati ambazo zimevumbuliwa duniani kutokana na mfumo wa Procuc. Kanuni
hizi zinaainisha jinsi malipo mbalimbali ya kifedha baina ya mweye mali na
mwenye hela na kwa timu ya Procuc yatakavyofanyika katika mfumo huu.
Jinsi
mfumo wa Procuc utakavyofanyika
Mfumo wa Procuc
utafanyika kwa kuchangia Procuc kama ifuatavyo:-
Mwenye hela atapaswa
kuchangia kiasi fulani cha hela kwenye Procuc kulingana na uwezo wake kwa
malengo ya kujipatia faida kutokana na pesa aliyochanga. Mchango ambao mwenye
mali anapaswa kuchangiwa na wenye hela ni asilimia themanini (80%) tu ya mtaji
wake. Kwa mfano, kama mwenye mali ana mtaji wa Tshs. milioni tano
(Tshs.5,000,000/=), anastahili kuchangiwa na wenye hela kiasi cha shilingi
milioni nne (Tshs.4,000,000/=) tu.Kwa hiyo asilimia themanini ya mtaji wa
mwenye mali inawezekana kabisa kurejeshwa kwa wenye hela. Faida ya mwenye hela
inatokana na kisasi cha hela ambacho atakuwa amechangia kwenye Procuc. Kwa mfano, endapo mwenye hela atachanga kiasi cha
laki tano (Tshs.500,000/=), kama mtaji wake, kwa muda wa miezi tisa, faida yake
itakuwa shilingi laki mbili thelathini na saba elfu na mia nne
(Tshs.237,400/=).Faida hiyo inatokana na asilimia 0.52 (0.52%) kama kiwango
ambacho kinatumika katika kukokotoa
kipato cha mwenye hela kwa siku na %CFP = 5%.Hata hivyo kiwango hicho
cha asilimia kinaweza kubadilika kulingana na hali halisi ya gharama za maisha
kwa kipindi hicho.Mabadiliko hayo hayatatokea kama tayari mkataba baina ya
mwenye mali na mwenye hela umekwishatiwa saini kwa ajili ya kuendesha
Procuc.Mkataba ukiisha, mwenye mali atarejesha mtaji pamoja na faida kwa mwenye
hela.Baada ya marejesho, mwenye hela anaruhusiwa kutia saini mkataba mwingine
kama yeye mwenyewe kwa hiari yake atahitaji kufanya hivyo.
USALAMA WA FEDHA YA
MWENYE HELA (CUSTOMER’S FINANCIAL SECURITY)
Kabla ya kuainisha
usalama wa fedha ya mwenye hela, goja
tuangalie mambo yafuatayo:-
·
Mchakato
wa kumpata mwenye mali((kwa ufupi), -rejea maelezo zaidi kwenye kitabu).
·
Usimamizi
wa Serikali, Benki na Timu ya mfumo wa Procuc katika mfumo wa Procuc.
·
Malipo
ya mwenye hela
Mchakato
wa kumpata mwenye mali (kwa ufupi)
Kama
nilivyotangulia kusema hapo awali kuwa, Procuc inategemea mwenye mali, sehemu husika,
mazingira ya kibiashara na aina ya biashara. Mwenye mali anapaswa kuwa
na nyaraka mbalimbali za biashara yake
kama vile business license (for sole proprietors), certificate of incorporation
(for companies), certificate of registration for Taxpayer Identification Number
(TIN), Statement of Estimated Tax Payable for the Year of Income and inspection
booklet.Vilevile anatakiwa kupata idhini kutoka serikalini ya kuendesha Procuc.
Mchango ambao mwenye mali anapaswa kuchangiwa na wenye hela ni asilimia
themanini (80%) tu ya mtaji wake. Ili mwenye mali aweze kuwalipa wenye hela
malipo yao bila kusuasua, kila bidhaa anayoiuza lazima aiuze kwa faida ya asilimia
thelathini (30%) mpaka asilimia arobaini (40%) ndani ya mwezi mmoja. Kwa mfano,
kama bei ya kununulia bidhaa ni Tshs.1,000/=, bidhaa itauzwa kati ya Tshs.1,300/=
mpaka Tshs.1,400/= au kama bei ya kununulia bidhaa ni Tshs.10,000/=, bidhaa
itauzwa kati ya Tshs.13,000/= mpaka 14,000/= au katika kila milioni moja
(Tshs.1,000,000/=), zinatakiwa Tshs.300,000/= mpaka Tshs.400,000/= kama faida
ya mauzo ya bidhaa mbalimbali kwa mwezi. Kwa maana nyingine biashara inatakiwa
kuwa na mzunguko mkubwa wa fedha kwa mwezi. Uzoefu wa mwenye mali katika
biashara na historia ya madeni katika mfumo wa Procuc unahitajika kujulikana. Kwa nini yatupasa kufahamu uzoefu na historia
ya madeni ya mwenye mali? Ili kuepuka kuanguka kwa biashara na kumnasua
mwenye mali kuingia katika janga kubwa la kufilisika. Mtaji wa mwenye mali
unapaswa kuwa mtaji ambao hautokani na madeni kutoka vyanzo vingine kama vile
benki, taasisi za fedha au kwa watu binafsi. Endapo kama mwenye mali atakuwa na
madeni kutoka vyanzo vingine vya fedha, hatapoteza sifa za kuwa mwenye mali,
ingawa italazimika kukokotoa mtaji halisi ili aweze kupata mchango wa asilimia
themanini (80%) tu ya mtaji wake kutoka kwa wenye hela.
Ikumbukwe
kuwa, yapo baadhi ya mambo ambayo yanaweza kusababisha kuanguka kwa biashara
kama vile matumizi mabaya ya fedha (yaani kutumia fedha zaidi kuliko uwezo wa
mtu kiuchumi au kufurahia zaidi kabla ya muda husika), usimamizi mbovu katika
biashara au ufuatiliaji hafifu katika kila kinachoendelea katika biashara,
kushindwa kujipatia mtaji toshelevu, kuanzisha biashara kwa mkopo bila mtaji
halisi, kumalizia kulipa deni la mkopo kwenye benki kwa kukopa pesa kutoka
vyanzo vingine vya fedha na kutumia fedha ya mkopo katika mradi mwingine
tofauti na maombi ya awali kuhusiana na mkopo. Katika mfumo wa Procuc, fedha
kutoka kwa wenye hela, lazima itumiwe na mwenye mali katika mradi husika. Maana
ikitumika vinginevyo, kuna uwezekano mkubwa kwa biashara kukwama au kuanguka
kabisa. Kwa hiyo, uaminifu, umakini, uwajibikaji na elimu ya ujasiriamali ni baadhi
ya mambo ya msingi katika ustawi biashara.
Usimamizi
wa Serikali, Benki na Timu ya mfumo wa Procuc katika mfumo wa Procuc
Ili mfumo wa Procuc
uweze kufanya kazi vizuri, ushirikiano mkubwa unapaswa ufanywe na Serikali,
Benki na Timu ya mfumo wa Procuc.Ushirikiano wa vyombo hivi vitatu unaweza
kuleta matunda kwenye mfumo. Vyombo hivi vina majukumu yafuatayo:
Serikali
·
Kukusanya kodi ya mapato.
·
Kutoa ruzuku kwenye Procuc, hasa pale
mwenye mali apatapo uwezo wa kujenga kiwanda.
·
Kutoa idhini kwa mwenye mali kuendesha Procuc.
Benki
·
Kurahisisha zoezi zima la kuendesha
mfumo wa Procuc kwa kuwaunganisha mwenye mali na mwenye hela.Mwenye hela
atakwenda Benki ili kumfahamu mwenye mali ambaye anaendesha Procuc.Majina yote ya wenye
mali yatakuwa benki husika, kwa hiyo
itakuwa rahisi kwa Benki kutoa huduma hiyo.
·
Kurahisisha zoezi la malipo kwenye
akaunti ya mwenye mali na mwenye hela.
Timu
ya mfumo wa Procuc
·
Kuelimisha jamii kuhusu mfumo wa Procuc.
·
Kufuatilia kwa ukaribu maendeleo ya
Procuc zote.
Malipo
ya mwenye hela (Customer’s financial payments)
Malipo ya mwenye hela
yamegawanyika katika sehemu kuu mbili, ambazo ni:
·
Malipo ya kawaida ya mwenye hela (Customer’s
normal financial payments)
·
Malipo ya mwenye hela yanayotokana na kuvunjika kwa
mkataba baina ya mwenye mali na mwenye hela (Customer’s financial
payments due to tiocalization)
Malipo
ya kawaida ya mwenye hela (Customer’s normal financial payments)
Kama nilivyotangulia
kusema hapo awali kuwa, endapo mwenye hela atachanga kiasi cha laki tano
(Tshs.500,000/=), kama mtaji wake, kwa muda wa miezi tisa, faida yake itakuwa
shilingi laki mbili thelathini na saba elfu na mia nne (Tshs.237,400/=).Faida
hiyo inatokana na asilimia 0.52 (0.52%) kama kiwango ambacho kinatumika katika
kukokotoa kipato cha mwenye hela kwa
siku na %CFP = 5% . Kwa hiyo kipato chake kwa ujumla kitakuwa Tshs.737,400/=kwa
kipindi cha miezi tisa. Hata hivyo si lazima mwenye hela kulipwa malipo yake
kwa muda wa miezi tisa, kuna uwezekano wa kulipwa kwa muda tofauti kulingana na
jinsi atakavyotia saini kwenye mkataba wakati wa mwanzo.
Jedwali lifuatalo,
linaonesha jinsi ambavyo malipo ya kawaida ya mwenye hela yatakavyofanyika kwa
nyakati tofautitofauti:
TND
|
y
|
ITND
|
CFT
|
CFP
in Tshs.
|
8.6
|
2
|
7
|
1Week
|
18,200
|
17.2
|
3
|
14
|
2weeks
|
36,400
|
34.25
|
4
|
30
|
1 Month
|
78,000
|
68.5
|
9
|
60
|
2 months
|
156,000
|
137
|
17
|
120
|
4 Months
|
312,000
|
274
|
4
|
270
|
9Months
|
702,000
|
Malipo kwa siku 270 ni
Tshs. 702,000/= na kwa siku 274 ni Tshs.737,400/=
Malipo
ya mwenye hela yanayotokana na kuvunjika
kwa mkataba baina ya mwenye mali na mwenye hela (Customer’s financial payments
due to tiocalization)
Malipo ya mwenye hela
yanayotokana na kuvunjika kwa mkataba baina ya mwenye mali na mweye hela (Customer’s
financial payments due to tiocalization)
yamegawanyika katika sehemu kuu tatu ambazo ni:
·
Malipo ya mwenye hela yanayotokana na kuvunjika kwa
mkataba baina ya mwenye mali na mweye hela-liosababishwa na mwenye mali
(Customer’s financial payments due to
tiocalization caused by a Procuc Operator)
·
Malipo ya mwenye hela yanayotokana na kuvunjika kwa
mkataba baina ya mwenye mali na mweye hela- liosababishwa na mwenye hela(Customer’s
financial payments due to
tiocalization caused by a Customer)
·
Malipo ya mwenye hela yanayotokana na kuvunjika kwa
mkataba baina ya mwenye mali na mweye hela - liosababishwa na Timu ya
mfumo wa Procuc(Customer’s financial payments due to tiocalization caused by Procuc System Team)
Malipo
ya mwenye hela yanayotokana na kuvunjika kwa
mkataba baina ya mwenye mali na mweye hela-liosababishwa na mwenye mali
(Customer’s financial payments due to tiocalization caused by a Procuc
Operator)
Malipo ya mwenye hela
kutokana na kuvunjika kwa mkataba baina yake na mwenye mali
-liosababishwa na mwenye mali yatategelemea kiwango cha asilimia (tiocalization
percentage) alichojaza wakati wa kutia saini mkataba. Angalia jedwali
lifuatalo:
The Procuc Operator
Tiocalization Table for CGF drawn from CFC=Tshs. 500,000/=, %CFPD = 0.52%, TND = 274 days and %CFP = 5%
Tiocalization Number (TN)
|
Tiocalization Percentage(TP)
in %
|
Incremental Percentage( )
in %
|
B
(i.e log10( ))
in %
|
P
in Tshs.
|
1
|
48
|
0.52
|
-0.283996656
|
740,000
|
2
|
49
|
1.52
|
0.181843587
|
745,000
|
3
|
50
|
2.52
|
0.40140054
|
750,000
|
4
|
51
|
3.52
|
0.546542663
|
755,000
|
5
|
52
|
4.52
|
0.655138434
|
760,000
|
6
|
53
|
5.52
|
0.741939077
|
765,000
|
7
|
54
|
6.52
|
0.814247595
|
770,000
|
8
|
55
|
7.52
|
0.87621784
|
7750,000
|
9
|
56
|
8.52
|
0.930439594
|
780,000
|
10
|
57
|
9.52
|
0.978636948
|
785,000
|
11
|
58
|
10.52
|
1.02201574
|
790,000
|
12
|
59
|
11.52
|
1.061452479
|
795,000
|
13
|
60
|
12.52
|
1.097604329
|
800,000
|
Where P stands for Customer’s payment due to
tiocalization caused by a Procuc Operator and b stands for tiocalization exponent.
Malipo
ya mwenye hela yanayotokana na kuvunjika
kwa mkataba baina ya mwenye mali
na mweye hela- liosababishwa na mwenye hela(Customer’s payments due to
tiocalization caused by a Customer)
Malipo ya mwenye hela
kutokana na kuvunjika kwa mkataba baina yake na mwenye mali
-liosababishwa na yeye mwenyewe yatafanyika kama ilivyoanishwa katika jedwali
lifuatalo:
The table for CGF and I drawn from CFC=Tshs. 500,000/=, %CFPD = 0.52% and %CFP
= 5% at various TNDs.
TND
|
NM
|
M
|
CGF
in Tshs.
|
CFL
in Tshs.
|
%CFL
|
CI
in Tshs.
|
I=CGF+CI
in
Tshs.
|
30
|
1
|
November-30
|
103,000
|
397,000
|
79.4
|
9819.33
|
112819.33
|
61
|
2
|
December-31
|
183,600
|
316,400
|
63.28
|
18384.48
|
201984.48
|
92
|
3
|
January-31
|
264,200
|
235,800
|
47.16
|
19480.35
|
283680.35
|
121
|
4
|
February-29
|
339,600
|
160,400
|
32.08
|
16481.92
|
356081.92
|
152
|
5
|
March-31
|
420,200
|
79,800
|
15.96
|
35016.67
|
455216.67
|
|
|||||||
182
|
6
|
April-30
|
498,200
|
1800
|
0.36
|
-
|
-
|
213
|
7
|
May-31
|
578,800
|
-
|
-
|
-
|
-
|
243
|
8
|
June-30
|
656,800
|
-
|
-
|
-
|
-
|
274
|
9
|
July-31
|
737,400
|
-
|
-
|
-
|
-
|
Usalama wa fedha ya
mwenye hela (Customer’s Financial Security)
Kwa kuwa kiwango
anachotakiwa kuchangiwa mwenye mali kutoka kwa wenye hela ni asilimia themanini
(80%) tu ya mtaji wake, kiwango hicho kinawezekana kabisa kurejeshwa kwa wenye
hela pamoja na riba yake. Kwa mfano, kama mwenye mali anamtaji wa shilingi
milioni mia tano (Tshs.500,000,000/=), mchango kutoka kwa wenye hela utakuwa
shilingi milioni mia nne (Tshs.400,000,000/=) na kuufanya mtaji wa mwenye mali
kuwa mlioni mia tisa (Tshs.900,000,000/=). Endapo asilimia 0.52 kama kiwango
ambacho kitatumika katika kukokotoa kipato cha wenye hela kwa siku na %CFP=5%,
faida itakayotokana na milioni mia nne kama mtaji wa wenye hela kwa kipindi cha
miezi tisa itakuwa shilingi milioni mia moja themanini na tisa, laki tisa na
elfu ishirini (Tshs.189,920,000/=). Kiwango hiki cha pesa ni sawa na ongezeko
la asilimia 47.48 ya mtaji wa wenye hela. Pia ongezeko hilo ni sawa na asilimia
37.984 ya mtaji wa mwenye mali. Chukulia kwamba mwenye mali anafanya biashara
bila ya yeye kupata faida, ila fedha zinazopatikana ni kwa ajili ya kuwalipa
wenye hela tu, ukweli ni kwamba mtu huyu ataweza kurejesha fedha hizo. Kwa
mfano, katika milioni mia nne (Tshs.400,000,000/=), kila mioni moja (Tshs.
1,000,000/=) inatakiwa kuwa na faida ya shilingi laki nne, sabini na nne elfu
na mia nane (Tshs.474,800/=) kwa kipindi cha miezi tisa. Kiwango hicho cha
faida kinakadiriwa sawa na shilingi hamsini na tatu elfu (Tshs.53,000/=) katika
kila milioni moja kwa mwezi. Hebu
tujiulize, hivi, inawezekana kweli
katika kila milioni moja kukosekana laki nne sabini na nne elfu na mia
nane(Tshs.474,800/=) kwa miezi tisa au shilingi hamsini na tatu elfu (Tshs.53,000/=)
kwa mwezi kwa ajili ya kuwarejeshea fedha zao wenye hela? Jibu,
la hasha!
Kwa kuwa timu ya mfumo
wa Procuc itakuwa na mamlaka ya kufuatilia kwa ukaribu maendeleo ya Procuc
zote, ikionekana kuwa kuna kila dalili kwa mwenye mali kuanza kupata hasara
katika biashara yake, itavunja mkataba baina ya mwenye mali na mweye hela ili
kuweza kuokoa upotevu wa fedha katika pande zote mbili, na itafanya hivyo kwa
kushauriana na Serikali pamoja na Benki husika. Hata kama timu ya mfumo wa
Procuc itaingilia kati mkataba baina ya mwenye mali na mweye hela, sharti,
mwenye mali lazima atalazimika kumlipa mwenye hela kiasi fulani cha riba na
mwenye hela atalazimika kulipa mutable
amount.Kwa hiyo, katika mazingira hayo fedha ya mwenye hela itakuwa salama
kabisa.
Customer’s entry fee
(kiingilio cha mwenye hela) and Mutable amount
Mwenye hela atapaswa
kutoa kiingilio kabla ya kuanza mkataba au siku ya kuanza mkataba, kiingilio
hicho kitawezesha shughuli zote za kibenki kutekelezwa.Vilevile atapaswa kutoa kiasi
kidogo kiitwacho “mutable amount” siku ya kumaliza mkataba.Mutable amount
itaiwezesha timu ya mfumo wa Procuc kujiendesha au kutimiza majukumu yake kwa
ufanisi zaidi.
FAIDA
YA MFUMO WA PROCUC KWA SERIKALI NA BENKI
Serikari itakusanya
kodi kubwa kutoka kwa wenye mali kwa kuwa kipato cha wenye mali kitazidi
kuongezeka. Vilevile Serikali itakusanya kodi kwa wenye hela pale watakapopata
uwezo wa kuanzisha biashara zao wenyewe baada ya kupata mtaji kutokana na mfumo
wa Procuc. Benki zitaweza kupata wateja wenye sifa ya kukopa kwa dhamana
(collateral).
ISTILAHI
Kuna Istilahi mpya ambazo zimepatikana
kutokana na mfumo wa Procuc. Istilahi hizi zimetokana na Lugha ya Kiingereza na
pia matamshi yake yanapatikana kwenye kitabu.
KITABU
Mfumo wa Procuc umepelekea
kuandika kitabu kiitwacho “PROCUC
SYSTEM”. Kitabu hiki kina sura nne ambazo ni:
·
Introduction to Procuc System
·
Procuc Operation and Business units
·
Poculization and Procuclization
·
Let us invest in Tanzania.
Utendaji kazi wa Procuc
unategemea sana matumizi ya mashine ziitwazo “Electronic Fiscal Devices (EFDs)”, kwa hiyo, maelezo kuhusu
matumizi ya mashine hizo yameelezwa kwa kina kwenye kitabu hicho.Fursa
mbalimbali za uwekezaji kama vile kilimo,
viwanda, madini, utalii, biashara, nishati, uchukuzi, teknohama n.k.vimeelezewa
ndani ya kitabu.Nunua kitabu uone jinsi mfumo ulivyo naTanzania ilivyotajiri.Pia
Monetary units za nchi mbalimbali
duniani zimeandikwa kwenye kitabu.Hii itawapa fursa watu wanaosafiri kwenda
nchi mbalimbali duniani kufahamu pesa inayotumika katika nchi husika kabla ya
kuanza safari.
Kwa ufupi, nunua kitabu cha Procuc System, ujifunze
mambo yafuatayo:
·
Dhana
inayohusu mfumo wa Procuc
·
Wadau wa
Procuc
·
Mwingiliano wa
Procuc
·
Triple Mechanism Model (TMM)
·
The fundamental raison d’être of Procuc
System
·
Masharti ya
jumla kwa ajili ya kupata mkopo kutoka kwenye benki
·
Jinsi mfumo wa
Procuc utakavyofanyika
·
Masharti ya kuendesha Procuc
·
Umuhimu wa
mfumo wa Procuc
·
Makundi ya
watu au watu wenye sifa za kuendesha Procuc
·
Makundi ya
watu au watu ambao hawastahili kuendesha Procuc
·
Matumizi ya
mashine ziitwazo “Electronic Fiscal Devices (EFDs)” katika
mfumo wa Procuc
·
Financial
transaction
·
Commercial transaction
·
Business units (Sole proprietorship,
Partnership, Joint stock companies (Public limited company and Private limited
company), Cooperatives, Public
corporation, Local authorities and Parastatal bodies)
·
Mlandano na
tofauti kati ya mfumo wa Procuc na Business units zingine
·
Dhana
inayohusu poculization na procuclization
·
Dhana
inayohusu proeperio, prosperio na tiocalization
·
Exponential Principle of Poculization
·
Kanuni mpya za kihisabati
·
Monetary units
·
Uwekezaji,
mazingira ya uwekezaji, sababu za kuwekeza na fursa za uwekezaji Tanzania.
ONYO: NI
MARUFUKU KUANZA KUTEKELEZA MFUMO WA PROCUC BILA YA
TAMKO LA SERIKALI.
No comments:
Post a Comment